Tatizo la maji katika mji wa Mokowe

Tatizo la maji katika mji wa Mokowe eneo bunge la Lamu Magharibi linatarajiwa kumalizika kufikia mwezi Julai mwaka huu.

Akiongea katika hafla ya ufunguzi wa shule ya chekechea ya Mokowe, gavana wa kaunti ya Lamu Issa Timamy amesema kuwa serikali ya kaunti inaendelea kushughulikia suala hilo hadi pale wananchi wataakapoweza kupata maji safi ya kunywa.

Wakazi wa Mokowe kwa sasa wanatumia maji safi kutoka kwa gari za kusambaza maji ambapo pia miji mingine inayokumbwa na tatizo hilo inapelekewa.

Kufikia sasa serikali ya Lamu imetatua tatizo la maji katika sehemu tofauti za Lamu Mashariki na Magharibi.

Trackback from your site.

Leave a comment

*