Manda settlement scheme kaunti ya Lamu

Mwenyekiti wa tume ya ardhi nchini Profesa Muhammad Swazuri amezindua rasmi mpango wa makazi wa kisiwa cha Manda au Manda settlement scheme kaunti ya Lamu.

Katika kikao na wenyeji wa sehemu hio ambapo pia viongozi wa serikali ya kaunti ya Lamu akiwemo naibu gavana Eric Mugo na seneta Abu Chiaba wamehudhuria, Swazuri amesema kuwa watakao faidi katika mpango huo ni jumla ya watu 375 walioorodheshwa tangu mwaka 2011.

Kulingana na Swazuri huenda wakazi hao walioorodheshwa katika mpango huo wakapata hekari sita au nne za shamba badala ya nane kama ilivyokubalianwa awali kufuatia mapendekezo mawili kwa ajili ya kupanga mji.

Zoezi hilo linalofuata agizo la mahakama limetangazwa kuanza rasmi baada ya kusitishwa oktoba mwaka jana.

Trackback from your site.

Leave a comment

*