Mswada wa kumtoa Amina Rashidi ni dhana za kisiasa, asema Gavana Timamy

Gavana wa Lamu Issa Timamy amevunja kimya chake leo kuhusu mswada uliopitishwa na wajumbe wa bunge la Lamu linaloongozwa na spika Mohammed Hasheem wa kumtaka Waziri wa ardhi Amina Rashid kufanyiwa uchunguzi kwa kile kinachodaiwa kutowajibika katika kazi zake.

Akizungumza na wanahabari Timamy amesema tangu serikali ya Ugatuzi takribaan wakaazi 5000 wa Kaunty hiyo wamejipatia hati miliki tangu Kenya kujinyakulia uhuru kupitia wizara inayoongozwa na waziri Amina Rashid, akasema kuwa hizo ni dhana za kisiasa.

Mswada huo ulioletwa bungeni na kiongozi wa walio wengi katika bunge hilo Abdu Kassim lilipitishwa, na Waziri wa ardhi Amina Rashid atafanyiwa uchunguzi kubaini ukweli katika kile kinachodaiwa kutowajibika katika kazi zake au la.

Trackback from your site.

Leave a comment

*