Usajili wa kura katika kaunti ya Lamu

Lamu, KENYA: Tume huru uchaguzi na mipaka nchini IEBC imefikia siku ya pili katika kaunti ya Lamu kusajili watu kama wapiga kura, baada ya kusitishwa kwa mda, kufautia kesi iliokuwa kotini kati ya Gavana wa lamu Issa Timamy na aliyekuwa mgombea wa kiti cha ugavana wa uchaguzi wa mwaka 2013 Fahim Twaha.

“Katika mazungumzo yangu na baadhi ya maafisa wa usajili katika vituo mbali mbali katika kaunti hii, wamesema kuwa tofauti ya jana na leo watu hawakujitokeza kwa wingi hivyo basi leo wanatarajia wakaazi kujitokeza kwa wingi na kujisajili kama wapiga kura, na kuwataka kuepuka dharura ya usajili wakati wa mwisho.” Gavana Timamy akizungumza na wanahabari

 

“Niliwahi kuzungumza na mmoja wa wakaazi wa Lamu ambaye amejitokeza katika shughuli ya kukata kura na hakuficha furaha yake, hatimaye kupata fursa ya kusajiliwa kama wakenya wengine.” Asema Timamy

Trackback from your site.

Leave a comment

*