Soko la Utalii kuimarika kaunti ya Lamu

Lamu

Serikali ya kaunti ya Lamu imeandaa kikao na washikadau mbali mbali katika sekta ya utalii akiwemo balozi wa Ufaransa humu nchini Emamanuel Renoult katika kujadili mikakati kabambe kuhakikisha soko la utalii katika kaunti hii itapanda kwa asilimia kubwa kufuatia kuzorota kwa uchumi kwa ukosefu ya watalii.

Akizungumza na waandishi wa habari Gavana wa Lamu Issa Timamy amesema serikali ya kaunti inafanya kila jitihada katika kuimarisha hali ya usalama katika kaunti hii, kwa ushirikiano na afisi ya kamishna wa kaunti hii Joseph Kanyiri.

Aidha waziri wa utalii wa kaunti Samia Omar Mbwana amesema wana matumaini kwa nchi za ughaibuni kutoa ruhusa kwa raia wao kuja kutalii Lamu ili uchumi uweze kuendelea, na wengi wa vijana kupata ajira, kwani idara ya utalii ndio mojawapo ya kitega uchumi wa vijana katika kaunti hii.

 

Story by Alwasila

Trackback from your site.

Comments (2)

 • Avatar

  simon murimi

  |

  kindly get my cousin a 3months industrial attachment… he has completed adegree in tourism n hospitality

  Reply

  • Avatar

   Ali Ahmed

   |

   Hi Murimi, ask him to visit Tourism offices at Lamu town see if he can be help.

   Reply

Leave a comment

*