Kaunti ya Lamu yapokea boti mbili kutoka shirika la Al-kheir

Shirika la Al-Kheir foundation kwa ushirikiano na serikali ya kaunti imetoa boti mbili kwa hospitali kuu ya Lamu ya kusaidia kuwahudumia wagonjwa wakati wa dharura.

Akizungumza wakati wa sherehe iliyoandaliwa katika Hospitali kuu ya kaunti Gavana wa Lamu Issa Timamy amesema boti moja itahudumia wagonjwa wanaokuja katika hospitali ya lamu na nyengine itatumika lamu mashariki.

khair

MOJAWAPO YA BOTI ILIYOTOLEWA NA SHIRIKA LA AL-KHAIR KWA WIZARA AFYA YA LAMU KATIKA SHEREHE ILIYOANDALIWA HOSPITALI KUU YA LAMU, 4 TH JUNE 2016

Wakati huo huo mwakilishi kutoka shirika la Al-kheir Mohammed Tarik ameishukuru serikali ya kaunti kwa ushirikiano mzuri na kuahidi kuleta kheri nyingi katika kaunti hii siku za usoni.

Haya yamejiri wiki mbili baada ya mama wa Taifa Margaret Kenyatta kuzuru kaunti hii na kutoa gari ya kuzunguka kuwatibu wagonjwa katika mpango wa beyond zero campaign mjini Mokowe.

Itakumbukwa shirika la Al-kheir wanaendeleza shughuli ya kuwajengea vyumba vya kisasa wakaazi wa vijiji vya Ba Hamisi na Kiangwi Lamu Mashariki.

Trackback from your site.

Leave a comment

*