Shughuli ya kusafisha mji kwa minajili ya sherehe za Eid-ul-Fitr imeshika mkondo wake wa kwanza katika kaunti ya Lamu

Shughuli ya kusafisha mji kwa minajili ya sherehe za Eid-ul-Fitr imeshika mkondo wake wa kwanza katika kaunti ya Lamu kupitia wizara ya Elimu, vijana na mambo ya jamii, chini ya usimamizi wa afisaa wa ngazi ya juu katika wizara hiyo bi Hafswa Diffin.

Shughuli hiyo ambayo imeanza mapema hii leo inatarajiwa kuendelea kwa takriban muda wa siku tano  kuhakikisha usafi utadumishwa na zaidi kutoa ajira kwa vijana.

Msimamizi wa vijana wa kaunti ya Lamu Faiz Fankupi ameipongeza idara yake kwa kuwajali vijana na kuwapa kipao mbele katika maswala ya kutoa ajira.

 

Story by Al-wasila

Trackback from your site.

Leave a comment

*