Kuondolewa ushuru kwa bidhaa ya ‘Tende’

Gavana wa Lamu Issa Timamy ametoa shukrani kwa rais Uhuru Kenyatta kwa kuamuru shirika la KRA kutoa ushuru kwa Tende haswa Waislamu wanapoingia katika huu mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Akizungumza wakati wa kuadhimisha miaka 53 tangu Kenya Kujinyakulia uhuru wake Timamy amesema hii itakuwa afueni na itawezesha waislamu kupata tende kwa urahisi kwote nchini na haswa kwa wakaazi wa kaunty hii.

Wakati huo huo Timamy ameitaka idara ya usalama kupunguza vizuizi vya  barabara ya Lamu-Mombasa kwa wasafiri, hii ni baada ya kupokea malalamishi kutoka kwa wakaazi wa kaunty hii kutokana na uzito wa safari na kuchelewa.

Itakumbukwa wakati waziri wa usalama na mambo ya ndani Joseph ole Nkaissery alipozuru Lamu, katika mkutano uliofanywa ukumbi wa Lamu Fort, Timamy aliomba vizuizi vya barabara kuondoshwa na ombi lake lilikubaliwa, na baadae kurejea katika hali ya kawaida kwa hofu ya usalama.

Hata hivyo kufikia sasa idara ya usalama imeweka mikakati kabambe katika kuimarisha usalama katika kaunty hii.

Trackback from your site.

Leave a comment

*