Wizara ya utalii ya serikali ya kaunti Lamu imetoa vyeti takriban 300 kwa wanafunzi

Wizara ya utalii ya serikali ya kaunti lamu imetoa vyeti takriban 300 kwa wanafunzi waliofuzu katika mafunzo ya kuboresha utalii Lamu na Kenya nzima kwa jumla katika ukumbi wa Lamu Fort.

Akizungumza katika warsha hiyo ilodhaminiwa kwa ushirikiano wa tourism fund na wizara ya utalii wa kaunty ya Lamu naibu gavana Erick Mugo ameahidi ushirikiano mwema baina ya washikadau wa sekta ya utalii na serikali ya kaunti.

DSC_3903

Aidha mkurugenzi katika wizara hiyo Ali Ahmed ameipongeza hatua ya shirika la Tourism Fund kwa kuzidi kufanya kazi kwa karibu na wizara yake ili kuinua sekta ya utalii katika kaunti hii.

 

Story by Al-wasila

Trackback from your site.

Leave a comment

*