Gavana wa Lamu akagua miradi mbali mbali

Wizara ya afya Kaunti ya Lamu inayoongozwa na Dkt Mohamed Kombo  inaendeleza ujenzi  wa zahanati na ukarabati wa hospitali katika meneo mbali mbali ya Kaunti hiyo.

Akizungumza na wanahabari Kombo amesema wizara yake inafanya upanuzi wa hospitali mbali mbali katika Kaunti hiyo ikiwemo hospitali kuu ya Kaunti King Fahad pamoja na ya Witu ambapo imeongeza jengo la wagonjwa wa dharura  na maabara.

Katika ziara iliyojumuisha Gavana wa Lamu Issa Timamy pamoja na maafisa wengine wa serikali, Kombo amesema vifaa vipya vya kupimia wagonjwa vimegawanywa katika baadhi za hospitali katika Kaunti hiyo, mojawapo ikiwa ni Digital Paperless X-ray machine, ambayo itawawezesha wagonjwa kutibiwa hapa, kinyume na hapo awali iliyowalazimu kusafirishwa Kaunti  zingine.

Story nyingine

H.E Governor Timamy officially opening Matondoni sea wall, Lamu Kenya. 2016/07/23

H.E Governor Timamy officially opening Matondoni sea wall, Lamu Kenya. 2016/07/23

Timamy amewataka wakaazi wa Matondoni kuwa na subra na kuwahakikishia maendeleo mbali mbali katika eneo hilo licha ya bajeti ya Kaunti hiyo kuwa na mvutano baina ya Kaunti na Bunge .

Timamy ameyasema haya wakati wa sherehe ya kuzindua rasmi ngome eneo la Matondoni ambayo kwa mda mrefu imekuwa changamoto kwa wakaazi wa eneo hilo haswa wakati wa mvua na kusababisha mafuriko na uharibifu wa mali.

Haya yamejiri siku chache baada ya Bunge la Lamu kufanya mkutano ulowahusisha viongozi kutoka tabaka mbali mbali ikiwemo baraza la maimamu nchini CIPK tawi la Lamu, ambapo wametaka ushirikiano baina ya pande hizo mbili kuja na suluhu ambayo itanufaisha wananchi na maendeleo katika Kaunti hiyo.

 

 

Trackback from your site.

Leave a comment

*