Maendeleo ya Vijana Kaunti ya Lamu

Kikundi cha vijana, Jubilee Youth Group kutoka Mpeketoni, Lake Amu eneo bunge la Lamu Mashariki wana sababu za kutabasamu kwa kupokea mbegu na vifaa vya kulimia pamoja na piki piki 10 kutoka kwa Serikali ya Kaunti itakayowasaidia katika usafirishaji wa bidhaa hizo kuwafikia wanunuzi.

 Akizungumza wakati wa kuzindua rasmi mradi huo, Naibu Gavana wa Kaunti hiyo, ambaye pia ni waziri wa kilimo, Erick Mugo amelitaka kundi hilo la vijana kuwa na ushirikiano mzuri baina yao ili kuweza kuwafikia malengo ya kuuza bidhaa zao ndani na nje ya Kaunti.

 Wakati huo huo Gavana wa Kaunti hiyo Issa Timamy, amewapongeza  vijana hao  na kuwataka vijana zaidi kuiga mfano huo utakao toa ajira kwa wengi kwa kuunda makundi yatakayowasaidia katika siku zao za usoni.

Trackback from your site.

Leave a comment

*