Timamy amelitaka bunge la Lamu kupitisha mswada wa bajeti wa huu mwaka

Gavana wa lamu Bw. Issa Timamy amewataka wajumbe wa bunge la lamu kuwa na ushirikiano na serikali ya kaunti na kuweka tofauti zao mbali, na kuwatumikia wananchi kufuatia mvutano ambao unaendelea wakupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017.

Akizungumza na wanahabari Timamy amekanusha madai kuwa bajeti isipitishwe na badala yake amelitaka bunge la lamu kupitisha mswada wa bajeti  wa huu mwaka wa kifedha kwa maendeleo ya wananchi wa kaunti hiyo.

Wakati huo huo spika wa bunge hilo Mohammed Hashim amekana madai ya kutokuwa na ushirikiano na serikali ya kaunti aidha ameongezea kwa kusema kuwa, kulingana na katiba ya Kenya  kifungu cha 134 bunge linaweza kupitisha mswada wa bajeti  kwa asilimia 50% ya kukidhi mahitaji ya wananchi kabla ya bajeti kamili kupitishwa.

Trackback from your site.

Leave a comment

*