Archive for August 9, 2016

MCAs wakanusha madai kuwa wamepitisha mradi wa coal

Kikao cha kwanza cha kujadili Repoti ya EIA kimefanyika bunge la Lamu hii leo(2016/08/09) na kwanza MCAs walijisafisha na kudhibitishwa kuwa bado hawajapitisha mradi bali walipitisha fikra ya kujengwa mradi iwapo maadili ya usalama yatazingatiwa.

Pili bunge wameapa kupinga mradi iwapo hakutokuwa na maandishi ya maagano juu ya usalama wa jamii, ajira kwa jamii na afya kwa jamii, pia wameomba mda wa ziada kujadili repoti hiyo kwa pupitia wataalamu wao watakao waamini.

Amu power wameahidi hayo kufanyika ukumbi  na repoti ilowasilishwa imeonyesha madhara asilia yatadhibitiwa ipasavyo.

Kikao cha pili kitafanyika ukumbi wa KPA, Lamu  leo mchana(2016/08/09) kupokea mapendekezo ya technical na community committees.