Archive for August 12, 2016

Kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la NEMA ni kwamba usalama wa wananchi wa eneo hilo umethibitiwa ipasavyo

Shirika la Amu Power kwa ushirikiano na wizara ya Kawi limeandaa vikao mbali mbali katika Kaunti ya Lamu kuwafahamisha wakaazi kuhusiana na ripoti kutoka kwa shirika la NEMA ambayo ilikua inasubiriwa na wakaazi hao, mradi unaotarajiwa kuzalisha umeme kutumia moto wa makaa.

 Kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la NEMA ni kwamba usalama wa wananchi wa eneo hilo umethibitiwa ipasavyo, na ripoti hiyo imefanyiwa utafiti na wataalam tofauti kutoka nchi za Afrika Kusini na Uingereza ni kuwa mradi utajengwa kwa teknolojia ya kileo ambayo haitakuwa na madhara kwa afya ya mwanadamu na viumbe vingine.

DSC03755

Viongozi wa dini wajumuika kuhudhuria kongamano kuu liloandaliwa na shirika la Amu Power

 Katika ziara hiyo ya siku nne shirika la Amu Power limefanya mikutano iliowajumuisha viongozi kutoka tabaka mbali mbali kama vile baraza la maimamu, vikundi vya jamii, vikundi vya kina mama, na vile vile wajumbe wa Bunge la Lamu ambao wameapa kuupinga miradi iwapo hakutokuwa na maandishi ya maagano MOU (Memorandum Of  Understanding) juu ya usalama, ajira na afya kwa jamii.

 

Story by Al-wasila