Mjumbe maalum wa Bunge la Kaunti ya Lamu Bi. Amina Kale amewataka wazazi kutilia mkazo elimu ya dini pamoja na ya dunia kwa watoto

Mjumbe maalum wa Bunge la Kaunti ya Lamu Bi. Amina Kale amewataka wazazi kutilia mkazo elimu ya dini pamoja na ya dunia kwa watoto wao na kuwafunza maadili, uongozi bora na kudumisha amani baina yao.

Akizungumza wakati wa sherehe ya mashindano ya kusoma Quran, Mashairi na Khutba iliowajumuisha wanafunzi  iliodhaminiwa na chama cha KIKOZI,  Kale amesema wanatarajia kuunda vikundi mbali mbali ambavyo vitawawezesha wanafunzi kuhamasisha kuhusu amani na vitakavyosaidia maendeleo ya madrasa.

Mjumbe maalum wa bunge la Kaunti ya Lamu, Bi Amina Kale 2016/09/26 Photo Alwasila

Mjumbe maalum wa bunge la Kaunti ya Lamu, Bi Amina Kale 2016/09/26 Photo Alwasila

Wakati huo huo mwenyekiti wa baraza la Maimamu na wahubiri nchini Kenya CIPK tawi la Lamu Sheikh Abubakar Shekue amewapongeza wanafunzi wote kwa jumla na kuwahimiza watie bidii na vile vile katika masomo ya dini itakayowaisidia katika maisha ya leo na akhira.

Trackback from your site.

Leave a comment

*