Shirika la Amu Power limeandaa kikao kingine kujadili mradi wa coal

Shirika la Amu Power limeandaa kikao na wajumbe wa bunge la Lamu kilichowajumuisha waakilishi kutoka wizara ya KAWI, Tume ya ardhi ya Kitaifa, shirika la umeme na mwakilishi kutoka African Development Bank  kutoa mapendekezo na kutathmini kuhusu umuhimu na madhara ya kiwanda cha Kwasasi.

Katika kikao hicho, wajumbe wa Bunge hilo wamekanusha madai kuwa walipitisha mswada wa kuendeleza mradi  na kulitaka shirika la Amu Power  kuwapeleka kuenda  kushuhudia mradi wa coal ulioko nchini China na Afrika Kusini ili kuhakikisha usalama wa mazingira na afya.

Wakati huo huo mmoja katika wakulima wa eneo la kwasasi Halima Majid amewataka wajumbe wa bunge la Lamu kuenda kuangalia na kutambua maslahi ya mkulima wa eneo la Kwasasi, kabla ya kuenda kuangalia miradi ilioko Ughaibuni.

 

 

Story by Al-wasila

Trackback from your site.

Leave a comment

*