Wakulima wa eneo la kwasasi Kaunti ya Lamu wamemnyoshea kidole cha lawama mweneyekiti wa tume ya ardhi ya kitaifa Hussein Swazuri

Wakulima wa eneo la kwasasi Kaunty ya Lamu wamemnyoshea kidole cha lawama mweneyekiti wa tume ya ardhi ya kitaifa Hussein Swazuri baada ya kutokubaliana kuhusu kiwango cha fedha ambayo wanafaa kulipwa kama ridhaa ya mashamba yao ambayo yatatumiwa kujengewa mradi wa coal utakaozalisha umeme kwa kutumia moto wa makaa.

Akizungumza katika kikao kilichowajumuisha washikadau kutoka sekta mbali mbali, wakiwemo wakulima , waakilishi kutoka wizara ya Kawi, African Development Bank  na shirika la Amu Power Swazuri amesema kitita cha Shilingi 800,000 zitatolewa kwa kila hekari  kulingana na thamani ya ardhi hiyo ya Kwasasi, na kuwataka wakulima hao kufahamu kuwa katiba ya Kenya hairuhusu mradi kuanzishwa kama mkulima hajaridhika na ridhaa na ana haki ya kufungua mashtaka kotini.

Eneo la Kwawasasi, photo by Ali Ahmed

Eneo la Kwasasi, photo by Ali Ahmed

Wakati huo huo wakulima hao wameitaka Tume ya ardhi ya kitaifa inayoongozwa na Hussein Swazuri kuangalia maslahi yao licha ya kwamba wao ni maskini na pia wamesitishwa kulima katika mashamba hayo kwa takriban miaka miwili kufikia sasa.

 

Story by Alwasila

 

Trackback from your site.

Leave a comment

*