Wanafunzi 28 kutoka wodi ya Basuba wafaidika kupokea bursary ya shilingi 850,000 kutoka wizara ya elimu ya kaunti ya Lamu

Wizara ya elimu ya serikali ya Kaunti ya Lamu inayosimamiwa na waziri Hamis Kaviha imetoa hundi ya bursary ya shilingi 850,000 kwa wanafunzi 28 wanaosoma shule ya upili ya Mokowe wanaotoka katika jamii ya Awer, wodi ya Basuba.

Akizungumza kwenye kikao kilichowajumuisha walimu na wanafunzi, Gavana wa Kaunti ya Lamu Issa Timamy ameahidi kuwawekea maji na umeme  katika shule hiyo, na vile vile kuwapa changamoto wanafunzi hao kutoa matokea bora katika mtihani wa kitaifa K.C.S.E.

Itakumbukwa shughuli ya kutoa bursary kwa wanafunzi kuanzia shule ya upili hadi chuo kikuu imekuwa ikiendelea kwa mda, hii ni kuhahakisha kwamba kiwango cha elimu kitapanda kwa asilimia kubwa katika Kaunti hiyo.

 

Trackback from your site.

Leave a comment

*