Warsha ya kupeana mafunzo ya kufuatilia Tender yakifanyika katika ukumbi wa Maharusi, Lamu

Waakilishi kutoka Hazina ya Kitaifa kitengo cha ununuzi wameandaa kikao leo hii katika ukumbi wa Mahrusi kilichowajumuisha wanakandarasi kutoka Kaunti ya Lamu na kuwapa mafunzo ya kufuatilia tender  zinapotangazwa na vitu vinavyohitajika ya kumuezesha mtu kupata kazi hiyo.

Akizungumza kwenye warsha hiyo afisaa mkuu wa kitengo cha ununuzi Kaunti ya Lamu Bi. Jamila Masenzi ameitaka wizara hiyo pia izingatie maslahi ya mtoto kiume na kusisitiza ya kwamba endapo mtoto wa kiume hatafikiriwa katika jamii basi yuko katika hatari ya kujihusisha na mihadarati ambayo itamuathiri katika siku za usoni.

Wakati huo huo mmoja kati ya waakilishi kutoka kitengo cha ununuzi ya serikali kuu Enock Kirungu amewataka wanakandarasi hao kutumia njia mwafaka ya kuwawezesha kufaulu tender(zabuni)  ili kuepukana na kukataliwa kwa maombi yao.

Kwa mujibu wa vifungu takriban 200 ambavyo vinazungumzia kwa mapana kuhusiana na Zabuni ni kwamba asilimia 30 itatengwa kwa ajili ya kina mama, vijana na walemavu na asilimia 20 kwa minajili ya waakazi wa Kaunti ya Lamu.

 

Trackback from your site.

Leave a comment

*