Wizara ya fedha ya serikali ya Kaunti ya Lamu imewataka wamiliki wa ardhi wa Kaunti hiyo kulipa madeni ya kodi ya ushuru kabla ya tarehe 07/10/2016

Wizara ya fedha ya serikali ya Kaunti ya Lamu imewataka wamiliki wa ardhi wa Kaunti hiyo kulipa madeni ya kodi ya ushuru kabla ya tarehe 07 mwezi  wa 10 mwaka huu ili kuepuka kutozwa kwa ada ya ziada.

Kwa mujibu wa waziri wa fedha wa serikali ya Kaunti Atwaa Salim amesema kuwa  Kaunti hutangaza “waiver” kwa mwaka mara mbili kwa wenye madeni kusamehewa penalti zao. 

Wakati huo huo Atwaa amewataka wenye mashamba kufika ofisini na kuangalia statements za madeni yao na yeyote atakaepitisha mda uliowekwa ama kutolipa madeni hayo ndani ya siku kumi na tano hatua za kisheria zitachukuliwa

Trackback from your site.

Leave a comment

*