Wizara ya uvuvi ya serikali ya Kaunti ya Lamu imewataka wavuvi na wachuuzi wa samaki kuwa na subra

Wizara ya uvuvi ya serikali ya Kaunti ya Lamu imewataka wavuvi na wachuuzi wa samaki kuwa na subra wakati ambapo ujenzi wa chumba cha kuhifadhia samaki pamoja na coal store unaoendelea maeneo ya Kizingitini na Kiunga.

Afisaa wa ngazi ya juu katika wizara hiyo Abdalla Masoud amesema wizara yake imejiandaa kutafuta masoko ya ziada ya kuuza samaki kutoka Kaunti ya Lamu hadi Kaunti nyengine na kutarajia kiwango cha uvuvi kuongezeka kwa asilimia kubwa.

Masoud aidha amesema wizara yake imejiandaa kutoa mashini za maboti  zitakayowawezesha wavuvi kufika maji ya kina kirefu na kupunguza mda mwingi kama ilivyo kuwa hapo awali.

Itakumbukwa wizara hiyo inayoongozwa na Bi. Grace Mburu, imekuwa ikitoa mashini za maboti, na vifaa mbali mbali vya  kufanyia uvuvi kwa wavuvi wa kaunti hiyo.

 

Trackback from your site.

Leave a comment

*