Sherehe za kuadhimisha siku kuu ya Mashujaa

Sherehe za kuadhimisha siku kuu ya Mashujaa iliyofanyika lamu Fort Mkunguni, zikiongozwa na mstahiki Gavana wa County ya Lamu akiandamana nae mstahiki Naibu Gavana, muwakilishi wa wanawake bungeni, kamishna wa county ya Lamu, Mawaziri, wakuu wa usalama na wafanyikazi Wa serikali katika sherehe iliyovutia umanti.
Katika hotuba yake Muheshimiwa aliipongeza hotuba ya Rais wa jamuhuri ya Kenya H.E Uhuru Kenyatta iliyosomwa na County Kamishna, na kumtambua Raish kama shujaa wa nchi hii kwa kazi na jitihada za serikali yake katika kukuza county ya lamu, akimpongeza zaidi kwa kukitambua kikundi cha ngoma za asili cha Siu kwa mwaliko wake kutumbuiza katika sherehe ya mashujaa.

Wananchi wa County ya Lamu walitajwa kama Mashujaa katika kuteleza mambo ya kujenga umoja na ushikamano wao katika kuipeleka mbele County hii, aliwatambua Mashujaa wote waliohusika katika kukomboa na kutupatia Uhuru wa Nchi.

Mstahiki Gavana Issa Timamy aliwasihi wananchi kuishi kwa amani na ushikamano baina yao na kuwatahadharisha dhidi ya kugawanywa katika misingi ya kisiasa, aliwasihi wakaazi wa Lamu na wananchi wa Kenya Kwa pamoja kuwa mambo muhimu ni kuishi kwa amani, upendo na ushikamano wakati ambao Lamu na Kenya kwa jumla inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo hali ya ukame iliyo athiri maeneo makubwa katika County ya lamu.

Muheshiwa alitaja ukame kama changamoto katika County ya Lamu na kusema kuwa Serikali yake iko kifua mbele ikishirikiana na serikali kuu. Serikali ya County chini ya uongozi wake Mstahiki Gavana Issa Timamy imekuwa ikisambaza Maji katika sehemu zilizokumbwa na ukame katika County nzima na kuahidi kuwa Serikali yake ina mipango madhubutu katika kuzuwia janga hilo kuenea, katika bajeti ya mwaka huu Muheshimiwa ameahidi kutenga kiwango cha fedha kununua Mashini zitakazo tumuka kubadilisha maji ya chumzi na kutoa maji tamu zitakazopelekwa Siu na Kiunga ili kuzuwia hali ya ukame maeneo hayo.

Muheshimiwa Gvana alitoa onyo kwa watumiaji na wauzaji mihadarati kuwa, Serikali yake haitolifungia macho suala hilo, akisisitiza kuwa watakaopatikana na hatia wakamatwe na kuchukuli hatua za kisheria. Aliahidi kufanya kazi pamoja na idara za kiusalama, viongozi na washika dau mbalimbali ili kuhakikisha swala la mihadarati limekomeshwa na kudhibitiwa vilivyo. Aliahidi kukutana na viongozi hao katika mda wa wiki mbili zijazo kujadili na kutoa mwafaka juu ya swala hilo.

Trackback from your site.

Leave a comment

*