Wanaodaiwa Kunyakua Ardhi Shella Wafika Mbele ya NLC Kujitetea

Tume ya kitaifa ya ardhi nchini imewapa makataa ya wiki 2 wale wote wanaodaiwa kunyakuwa ardhi haswa sehemu za matuta ya mchanga katika milima ya Shella ambayo ndio chanzo kikuu cha maji safi kwa wakaazi wa kaunti ya Lamu, kuwasilisha stakabadhi zao za kuonyesha namna gani walipata hati miliki hizo la zivyo zifutiliwe mbali.
Akiongea na wanahabari baada ya wanaodaiwa kunyakuwa ardhi hizo kufika mbele ya tume hiyo ili kujitetea naibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Abigael Mbagaya Mukolwe amesema ni muhimu kwa sehemu za vyanzo vya maji kuhifadhiwa ili watu wasikose maji ya kunywa hasa wakati huu ambapo kumekuwa na ukame.
Mbagaya amesema katika kikao cha leo stakabadhi zilizowasilishwa zilikuwa na kasoro sihaba huku nakala nyingine zikiwa hazina sahihi ya msajili wa ardhi.
Ardhi ambazo zimesajiliwa kwa jina la kampuni kama vile Honey moon holdings ltd ziliwakilishwa na mawakili, ambao wengi wao waliiyomba tume ya kitaifa ya ardhi kuwapa mda zaidi wa kutafuta stakabadhi nyengine.
Wamiliki wa ardhi hizo walitakiwa kufika na letter of allotment, minutes approving allocation,copy of PDP, copy of a deed plan and copy of the title.
Nae msaidizi wa kibinafsi wa aliyekuwa mbunge wa Lamu magharibi Fahim Twaha, Paul Wainaina Kimani aliyemuakilisha alikuwa na wakati mgumu wa kueleza uhusiano wake na mteja wake huku akitakiwa aende kutafuta kutoka kwa mteja wake vipi alipata hati miliki hizo, huku tume ikiamuru kutojengwa jingo lolote katika ardhi hizo anazodaiwa kuchukua kinyume cha sheria.
Takriban watu mia moja wametakiwa kufika kwa tume ya kitaifa ya ardhi nchini ili kueleza ni vipi walipata hati miliki ya ardhi hizo ambazo ni vyanzo vya maji katika kaunti ya Lamu.
Tume hiyo itaendelea na vikao vyake hapo kesho katika ukumbi wa Lamu fort.

Trackback from your site.

Leave a comment

*