Makala Ya Mashine Za Boti Kwa Wavuvi Wa Lamu

Asilimia 80% ya wakaazi wa Lamu , hutumia uvuvi kama kitega  uchumi na raslimali  ya maisha yao.  Hivo basi kila kijiji cha kaunti ya Lamu mashariki, kimebobea kwa aina yake ya uvuvi, kama vile kiji cha kizingitini na kiwayuu  ni maarufu kwa uvuvi  wa kamba mawe na samaki wakubwa, kijiji cha Faza mbwajumwali na mtangawanda umaarufu wao ni wakuvua kaa na aina nyengine ya samaki.  Upande wa Lamu magharibi, eneo la matondoni linafahamika kama kambi ya uvuvi wa kamba wadogo.

serikali ya kaunti ya Lamu imepiga hatua katika kuboresha rasli mali hyo kupitia njia mbalimbali, ila katika makala ya leo nataka tuzungumzie mashine za boti zilizoweza kutolewa na kaunti ya Lamu kupitia idara ya uvuvi na mifugo kwa njia ya mkopo.

Takriban mashine 83 ziligawanyiwa wavuvi kupitia vyama vya BMU, vilivoko katika maeneo 19 ya  kaunti ya Lamu. Maeneo kama Shanga Rubu, Kiwayuu, Bandari salama, Siyu, Shanga Ishakani, Ndau, Myabogi, Mkokoni, Ishakani, Mbwajumwali, Kipungani, Pate, Matondoni, Kiunga, Shela, Faza, Amu na Kizingitini ndio walioweza kufaidika kwa mashine hizo.

 

Eneo la kizingitini ndilo lilopata mgao mkubwa wa mashine 16 kutokana na idadi kubwa ya wavuvi katika kijiji hicho huku maeneo ya amu na Faza ndio yaliofwata katika mgao kwa kupata  mashine 12 na maeneo yaliyobaki wakatunukiwa mashine 11.

Takriban asilimia  87% ya wavuvi waliopata mashine hizo wameweza kulezea faida kubwa wanayoipata kupitia mashine walizopewa katika shughuli zao za uvuvi, utafiti unaeleza kuwa wavuvi hao wamekuwa wakiweza kufikia maeneo yalio mbali kuvua samaki huku kiwango cha kupatikana kwa samaki kikiwa kimeongezeka kwazaidi ya kilo 20, vile vile wavuvi hao wameweza kupunguza mda wa usafiri kwa dakika sitini ikilinganishwa na zamani walipokuwa wakitumia matanga kwa usafiri wao.

Kulingana na idara husika, mradi huo utakuwa ukiendelea kila uchao kwa faida ya wavuvi wa Lamu.

Trackback from your site.

Leave a comment

*