Idara ya afya kaunti ya Lamu yapiga hatua kubwa

Sekta ya afya ni moja wapo ya sekta ambazo zimegatuliwa kutoka serekali ya kitaifa hadi zile za kaunti.

Kwa sababu hii serekali za kaunti zimetekwa jukumu la kusimamia sekta ya afya katika kila kaunti humu nchini.

Serekali ya kaunti ya Lamu ikiongozwa na msatahiki gavana Issa Timamy imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mwananchi haswa yule aliyoko mashinani amepata huduma ya matibabu popote alipo.

Kufikia sasa serekali ya kaunti ya Lamu imejenga na kuzifungua zahanati  nane katika maeneo mbali mbali ya kaunti ya Lamu huku nyingine mbili zikielekea kukamilika.

Zahanati hizi haswa zimejengwa katika maeneo ambayo wakaazi wake walikuwa wakitembea mwendo mrefu kutafuta matibabu na ni sehemu ambazo zilitengwa kwa mda mrefu.

Zahanati za hivi karibuni zilizofunguliwa rasmi na mstahiki gavana Issa Timamy ni ile ya uziwa na tewe tarafa ya Mpeketoni.

Nyingine ni Moa,Kastakakairu,Sinabiu, Maisha Masha na Ishakani huku zile za Bargoni na Kiangwi zikielekea kukamilika.

Zahanati hizi na zile yengine zilizotangulia kufunguliwa zina uwezo wa kujifungua akina mama kwani zimetegewa chumba maalum kwa shughuli hiyo kando na kutoa huduma nyingine.

Trackback from your site.

Leave a comment

*