Mabingwa wa kombe la gavana 2017

Timu ya wadi ya Mkomani ndio mabingwa wa mchuwano wa Kombe la gavana kaunti ya Lamu mwaka huu baada ya kuinyuka wadi ya Bahari ambao walikuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo,mabao matatu kwa mawili.

Mnamo dakika za mwanzo timu ya Bahari ilianza kuona lango na kufunga bao kupitia kwa Viterles kabla ya kukombolewa na Ahmed Athman wa timu ya wadi ya Mkomani.

katika kipindi cha pili Mahmud Athman alifungia timu ya Mkomani wadi bao la pili kabla ya kusawazishwa na Irungu wa timu ya Bahari.

Naye Issa Islam wa timu ya wadi ya Mkomani aliifungia timu yake bao la ushindi.

Ni mwaka wa tatu sasa tangu Kombe la gavana kaunti ya Lamu kuanzishwa na mstahiki gavana Issa Timamy.

Mwaka huu timu 160 ziliweza kushiriki dimba hili kutoka wadi 10 zaka kaunti ya Lamu.

mshindi alijiondokea na shilingi laki moja pesa taslim,mpira na jezi.

“Mungu akipenda mwakani fainali za Kombe hili la gavana zitachezwa huko Faza, Lamu Mashariki” Gavana Issa Timamy aliahidi.

Kauli mbiu ya Kombe la gavana Issa Timamy kaunti ya Lamu ni kuwaleta vijana pamoja na kuwahamasisha kutojiingiza katika utumizi wa dawa za kulevya.

Trackback from your site.

Leave a comment

*