Archive for June, 2017

Zahanati ya Muhamarani Wadi ya Mkunumbi

Zahanati hii ya Muhamarani ina hudumia watu wa sehemu ya Poromoko,Salama,Juhudi, Marafa,Mikinduni,Nyatha na Kaisari.

Kabla ya kujengwa kwa sehemu hii ya kujifungulia akinamama , kina mama wa sehemu hizi walikuwa wakitembea umbali wa kilomita 10 hadi 15 wanapotaka kujifungua na endapo kumetokea tatizo jambo ambalo lilikuwa linahatarisha usalama wa kina mama.

Gavana wa Lamu Issa Timamy aliwahimiza kina mama wajifunguwe hospitali ili wawezi kupata usaidizi wakati shida inapotokea.

Kadhalika gavana Timamy aliahidi kutoa shilingi elfu kumi kwa mama wa kwanza mja mzito atakaejifungua katika zahanati hiyo.

Zahanati ya Sinambio katika wadi ya Hongwe-Mpeketoni

Kufunguliwa kwa zahanati ya Sinabio katika wadi ya Hongwe tarafa ya Mpeketoni kumefikisha zahanati nane ambazo zimejengwa chini ya uongozi wa msatahiki gavana wa kaunti ya Lamu Issa Timamy.

Jengo la zahanati hiyo lilianza kujengwa na shirika moja la Rotary Club kutoka Italia na kushindwa kulikamilisha kwa sababu za kiusalama mnamo mwaka wa 2013.

Ukarabati wa jengo hili la zahanati uligharimu serekali ya kaunti ya Lamu shilingi milioni 8 katika mwaka wa kifedha wa 2016/2017.

Baada ya kukaa kwa mda kwa jengo hilo likiwa halikukamilika, serekali ya kaunti ilingilia kati na kulikarabati pamoja na kuweka vifaa ili iweze kupeana huduma kwa wakaazi wa Sinabio na maeneo mengine karibu.

Mara tu baada ya kufunguliwa rasmi  kwa zahanati hiyo na msatahiki gavana Issa Timamy huduma zikaanza kutolewa kwa wakaazi wa eneo hilo.

Zahanati hiyo ina chumba cha kujifungulia akina mama na iko na wahudumu wa afya wawili.