Zahanati ya Sinambio katika wadi ya Hongwe-Mpeketoni

Kufunguliwa kwa zahanati ya Sinabio katika wadi ya Hongwe tarafa ya Mpeketoni kumefikisha zahanati nane ambazo zimejengwa chini ya uongozi wa msatahiki gavana wa kaunti ya Lamu Issa Timamy.

Jengo la zahanati hiyo lilianza kujengwa na shirika moja la Rotary Club kutoka Italia na kushindwa kulikamilisha kwa sababu za kiusalama mnamo mwaka wa 2013.

Ukarabati wa jengo hili la zahanati uligharimu serekali ya kaunti ya Lamu shilingi milioni 8 katika mwaka wa kifedha wa 2016/2017.

Baada ya kukaa kwa mda kwa jengo hilo likiwa halikukamilika, serekali ya kaunti ilingilia kati na kulikarabati pamoja na kuweka vifaa ili iweze kupeana huduma kwa wakaazi wa Sinabio na maeneo mengine karibu.

Mara tu baada ya kufunguliwa rasmi  kwa zahanati hiyo na msatahiki gavana Issa Timamy huduma zikaanza kutolewa kwa wakaazi wa eneo hilo.

Zahanati hiyo ina chumba cha kujifungulia akina mama na iko na wahudumu wa afya wawili.

Trackback from your site.

Leave a comment

*