Archive for July 8, 2017

Kizingitini Youth Polytechnic Yafunguliwa Upya

Gavana wa Lamu Issa Timamy amekifungua upya chuo cha kiufundi cha vijana huko Kizingitini baada ya kuachwa kwamda mrefu na utawala uliopita.

Chuo hiko kilicho katika eneo bunge la Lamu mashariki kilijengwa na serekali ya ujarumani na badaye kuchukuliwa na serekali  ya Kenya na hatimaye kufungwa kutokana na usimamizi mbaya na kuharibika kwa miundo msingi yake.

Mafunzo ya kiufundi kama vile useremala,ushonaji wa nguo na masomo ya tarakilishi yalikuwa yakifundishwa.

Baada ya kujakwa serekali ya kaunti chini ya mstahiki gavana Issa Timamy chuo hiki kimekarabatiwa na  kupata sura mpya.

Chuo hiko kilichosajiliwa na wizara ya elimu sasa kinasimamiwa na serekali ya kaunti ya Lamu na kupata jina la Kizingitini Vocational Training Center.

Tayari vifaa vimewekwa na waalimu na mafunzo yanatarajiwa kuanza mara moja.

Akizungumza baada ya kufungua upya chuo hicho, gavana Issa Timamy amewarai wazazi kutoka eneo hilo na sehemu nyingine jirani kuhakikisha kuwa wamewapeleka vijana kwa mafunzo hayo hasa wale ambao hawakuweza kuendelea kimasomo kwa kupata alama za chini.