Archive for July 9, 2017

Vifaa Vya Uvuvi Vyatolewa Kwa Wavuvi Tchundwa

Wavuvi kutoka mjini Tchundwa eneo bunge la Lamu mashariki,hapo mano tarehe 7/08/2017 walinufaika na vifaa vya uvuvi kutoka kwa serekali ya kaunti ya Lamu.

Katika sherehe iliyoongozwa na mstahiki gavana Issa Timamy,wavuvi hao walipokea mashine za boti pamoja na mitungi yake,cooler box na mishipi ya kuvulia samaki.

Timamy amesema lengo lake ilikuwa ni kupeana machine za boti bila malipo lakini ndoto hiyo yake ili pingwa na baadhi ya wawakilishi wa kaunti.

Timamy ameongeza kusema kuwa kilichomsikitisha zaidi jambo hilo kwanza lilipingwa na aliyekuwa muwakilishi wa wadi ya Kiunga

Gavana Timamy amewaahidi wavuvi kuwa endapoatachaguliwa tena atahakikisha kuwa madeni hayo ya mashine za boti yatafutiliwa mbali.