Archive for July 13, 2017

Ramani Ya Maendeleo Ya Kaunti Ya Lamu Yazinduliwa

Serikali ya kaunti ya Lamu kupitia wizara ya Ardhi, Maji na Miundo msigi ikishirikiana na shirika la WWF imezindua rasmi ramani ya maendelo ya kaunti ya Lamu tarehe 12/7/2017 katika eneo la Mkunguni.
Kulingana na katiba ya Kenya ni lazma kwa kila kaunti kuwa na ramani ya maendeleao, nayo kaunti ya Lamu inayoongozwa na Gavana Issa Abdallah Timamy imeweza kuwa kaunti ya kwanza kutayarisha na kuzindua ramani hiyo.
Utayarishaji wa  ramani hii umechukua mda wa zaidi miaka miwili hadi kukamilika kwake na  imeigharimu serikali ya kaunti ya Lamu milioni thelathini(30Million).
Akiongea katika hafla hiyo, iliyohudhuriwa na Gavana wa Lamu na Naibu wake, maafisa wa National Land Commission, maafisa wa shirika la KWS na mawiziri tofauti kutoka serilaki ya kaunti ya Lamu, waziri wa Ardhi kaunti ya Lamu,Bi. Amina Rashid alisema kuwa ramani hiyo ni muhimu kwa kaunti ya Lamu kwani inatoa muongozo wa kutekeleza miradi na kuhifadhi rasili mali za kaunti hii.

Download Links for the Full Report:

VOLUME I_THE LAMU CSP MAY 2017_FINAL

VOLUME II_THE LAMU CSP MAY 2017_FINAL

VOLUME III_THE LAMU CSP MAY 2017_FINAL

VOLUME IV_GIS OUTPUT REPORT COMBINED