Witu Youth Polytechnic Yaboreshwa Zaidi

Witu Youth Polytechnic imepata taswira mpya tangu mstahiki gavana Issa TImamy kushika usukani wa kuendesha kaunti ya Lamu.

Kufikia sasa chuo hicho kimesajili wanafunzi wa taaluma mbali mbali 120 kutoka maeneo ya tarafa ya Witu na viunga vyake kaunti ya Lamu.

Pia waalimu zaidi wameletwa na kuajiriwa na serekali ya kaunti ya Lamu.

Taaluma zinazotolewa nimapoja na useremala,ushonaji wa nguo, umeme ,ujenzi wa nyumba miongoni mwa taaluma nyingine.

Chuo hiki kimenufaisha vijana kutoka vijiji vya Pangani, Maisha masha,Jipendeni,Chalaluma,Kastakakairu,Lumshi,Moa na Boko.

Na hii leo gavana Issa Timamy amekabidhi vifaa kwa chuo hicho cha kiufundi cha vijana Witu kama vile:-Computer 7, Virehani 9 na mashini ya kuchapisha makaratasi.

Timamy amesema ataendelea kukiboresha zaidi chuo hicho ili vijana waweze kupata taaluma za kiufundi.

Trackback from your site.

Leave a comment

*