Ajenda Zangu Kwa Watu Wa Lamu

Baada ya kula kiapo cha kuchukua usukani kama gavana wa jimbo la Lamu mnamo siku ya Ijumaa 18, Agosti, 2017, Muhishimiwa Fahim Yassin Twaha alihutubia halaiki ya watu eneo maarufu la mikutano ya kisiasa la Mkunguni.

Kwa ujumla hutba ya mstahiki gavana Fahim, ilisheheni wito wa umoja na amani na kuwataka wananchi wa Lamu kusahau yaliyopita katika ulingo wa kisiasa na badala yake kufanya kazi kwa bidii na upendo na kuahidi kuwatumikia wote kwa usawa ili kuipeleka mbele kaunti ya Lamu.

“Nawaahidi nyote, nitawatumikia nyote mulionipigia kura na ambao hamukunipigia kura, maanake nyote ni wananchi wa Lamu na nyote ni ndugu zangu na wanangu na nyote niwalipaji kodi ile huduma tunayowapa sio hisani nawafanyia, ni wajibu natekeleza” Fahim aliihakikishia hadhira.


Gavana Fahim aidha aliwapongeza viongozi wote waliochaguliwa pamoja naye akiwemo Rais Uhuru Kenyatta na kutaka ushirikiano na viongozi wote na hata wale walioshindwa.


Pia katika hutba yake Gavana Fahim alitaja mambo kadhaa ambayo atayapatia kipao mbele katika siku za mwanzo za uongozi wake kwenye serekali yake:-

1. Haja ya kusafisha mji wa Lamu.
2. Kuratibu upya usambazaji wa maji katika kaunti mzima ya Lamu kwa ushirikiano na serekali ya kitaifa.
3. Kuweka usalama baharini ili kupunguza ajali.
4. Kuweka helkopta ambayo itasaidia watu ikitokea dharura ya kiafya katika sehemu za mbali kama vile Kiunga.
5. Kuweka vifaa vya mawasiliano kwa kila chombo baharini.
6. Kuhakikisha kila mtoto katika kaunti ya Lamu amepata elimu hadi chuo kikuu.
7. Kuweka chuo cha mafunzo ya ubaharia na bandari.
8. Watoto elfu 10 kila mwaka watapata kazi.
9. Kuweka trola kwa wavuvi.
10. Kuwapimia ardhi watu wa Lamu.
11. Kuimarisha utalii.
12. Kuustawisha mji wa Manda.
13. Kuwaondolea deni wale waliopata machine za boti.
14. Kuweka feri katika eneo la Mtangawanda.
15. Kupunguza idadi ya wagonjwa wanosafirishwa kupata matibau ya ziada katika kaunti nyingine.

Trackback from your site.

Comments (1)

  • Avatar

    sirlim

    |

    that’s good congratulation Mheshmiwa governor,endeleza viunga uchumi kwa manufaa ya wana Lamu wote ondoa umasikin,na vijana wapatie ajira kwa wingi

    Reply

Leave a comment

*