Archive for September 21, 2017

Msaada Wa Kimapato Wa Ustawi Na Elimu Kutoka Kwa Shirika la Plan International

Nyumba 116 kutoka kaunti ya Lamu zimefuzu baada ya kupokea msaada wa kimapato wa ustawi na elimu kutoka kwa shirika la
Plan International kwa ushirikiano na shirila la USAID chini ya muavuli wa mpango wa “NILINDE”.

Mpango huo wa NILINDE ulikuwa unalenga kuzisaidia familia zenye watoto mayatima na zile ambazo zina watu ambao wako katika hali hatarishi katika kaunti ya Nairobi na Pwani.
Watoto hao pamoja na familia zao wamefaidika na karo za shule,sare pamoja na kupewa mifugo ili kujikimu kimaisha.
Familia hizo 116 ni za kwanza kufuzu kutoka kwa zaidi ya familia 2000 kutoka kaunti ya Lamu.

Akihudhuria sherehe za mahafali kwenye familia hizo gavana wa Lamu Fahim Twaha amewashukuru wahisani hao kwa niaba ya familia zao kwa kazi yao mzuri.
Aidha amewashukuru wazazi kwa kuwakaribisha wahisani hao majumbani mwao.

Wakati huo huo gavana Twaha ameyashukuru mashirika ya Akhghan na World Vision kwa kukubali kuupokea mradi huo ili kuuwendeleza baada ya mda wa watangulizi wao kukamilika.
Wale walionufaika na mradi huo na kufuzu walipokea shada kutoka kwa shirika hilo la Plan International.

Gavana Wa Lamu Akutana Na Wahundumu Wa Afya Katika Hospitali Ya King Fahad

Gavana wa Lamu Fahim Twaha amekutana na wahudumu wa afya katika hospitali ya King Fahad na kutaka kusikia kilio chao kufuatia mgomo wa wauguzi na maafisa wa kiliniki unaoendelea.

Wakitoa malalamishi yao wafanyikazi hao wa afya wamemuelezea gavana Twaha kuwa hawakuridhishwa na mabadiliko yaliyofanywa na tume ya kukadiria mishahara ya wafanyikazi wa umma (SRC)ambapo wameteremshwa daraja.

Aidha wamemuelezea gavana Twaha kuwa tume hiyo ya kukadiria mishahara imewapatia mambo ambayo hawakuitisha.

Wafanyikazi hao wa afya wamemtaka gavana Twaha kuchukua malalamishi yao na kuyawasilisha kwa baraza la magavana nchini  ili yazingatiwe.

Kwa upande wake gavana Twaha amewahakikishia wafanyikazi hao kuwa atafanya kila liwizalo kuhakikisha kuwa matakwa yao yamezingatiwa.

Aidha gavana Twaha ametoa wito kwa  wafanyikazi hao wa afya kutumia njia ya mazungumzo kwanza kabla ya kuchukua hatua za kugoma.

Twaha amesema mlango wake uko wazi na wakati wowote wanapomuhitaji yuko tayari kuwasikiliza.

Baada ya kikao hicho na wafanyikazi wa sekta ya afya katika hospitali ya King Fahad gavana Twaha alifululiza hadi katika hospitali ya Mpeketoni ili kukutana na wafanyikazi wake.

Aidha hapo kesho atatembelea hospitali ndogo ya kaunti huko Faza.