Archive for September 25, 2017

Maonyesho Ya Takataka Za Plastiki Katika Kaunti Ya Lamu

Maonyesho ya takataka za plastiki kwa mara ya kwanza yamefanyika katika kaunti ya Lamu kwenye ukumbi wa makavazi ya Lamu.

Maonyesho hayo yaliyofahamika kama Takataka Exhibition Lamu Fort,ni ya kuonyesha taka za plastiki zilizokusanywa katika fuo za bahari na watu wanaojitolea kufanya usafi baharini iliyowajumuisha baadhi ya vijana wa Lamu na wageni wanaoishi Lamu kutoka ngambo kwa ushirikiano na makavazi ya Lamu.

Akizungumza kama mgeni wa hishma katika maonyesho hayo gavana wa Lamu Fahim Twaha alifurahishwa na watu hao kuja na fikra hiyo ya kuhifadhi mazingira na kuwapongeza.

Twaha ametoa wito kwa wakaazi wa Lamu kuhifadhi mazingira na kutotupa taka ovyo ovyo. Wakati huo huo Gavana Twaha ametangaza kuwa atawaajiri kazi vijana waliojitolea kusafisha fuo za bahari wakiongozwa na Hassan Obo aliyejitolea kwa kazi hiyo kwa miaka 18.

Sherehe hiyo pia ilijumuisha wanafunzi wa shule za msingi za Lamu kwa kuwapa mafunzo ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira ambapo waliofuzu walikabidhiwa shahada.

Gavana Wa Lamu Fahim Twaha Akiwa Katika Hospitali Ndogo Ya Faza

Gavana wa Lamu Fahim Twaha akiwa katika hospitali ndogo ya Faza akikutana na wafanyikazi wa hospitali hiyo ili kusikia kilio chao kufuatia mgomo unaoendelea. Wakitoa malalamishi yao muhudumu mmoja wa maabara alisema kuwa wao wanafaa kupatiwa marupurupu ya wito wa dharura kama vile wenzao madaktari. Naye gavana Twaha aliwasihi wahudumu hao wa afya kurudi kazini huku akisema kuwa anawashughulikia licha ya kuwa maswala yao yako kwa SRC.

Wavuvi Wa Matondoni Wapata Huduma Za Kawaida Kwa Mashini Za Boti

Idara ya uvuvi kaunti ya Lamu ikiongozwa na mkurugenzi wake Kamalu Shariff ikishirikiana na kampuni ya kuuza mashine za boti ya Captain Andy’s Fishing Supply Ltd wakiwa na wavuvi wa Matondoni ili kupeana huduma za kawaida kwa mashine zilizopeanwa na serekali ya kaunti kwa mkopo.

Huduma hizo zimepeanwa kwa bai nafuu ili kuwasaidia wavuvi hao pamoja na kuwahamasisha dhidi ya kuzifanyia huduma za kawaida mashine hizo kila mda unapohitajika .

Wavui hao wameishukuru kaunti ya Lamu kwa huduma hiyo muhimu . Mashine hizo zilipeanwa kwa mkopo na serekali ya kaunti na sasa kupitia uongozi wa gavana Fahim Twaha ametangaza
kuwa atafutilia mbali madeni hayo.