Sherehe Ya Mashujaa Day 2017

Sherehe ya Mashujaa Day iliofanyika tarehe 20/10/2017 katika eneo la Mkunguni mjini Lamu ikihudhuriwa na Muheshimiwa Gavana Fahim Twaha akiwa pamoja na naibu wake Abdulhakim Aboud,Mwakilishi wa wanawake Ruwaida Obo na mwakilishi wa kata ya Mkomani Yahya Mohamed pamoja viongozi mbali mbali wa serekali kuu. Gavana katika hotuba yake alisisitiza kuweko kwa amani katika maregeleo ya uchaguzi wa urais utakaofanyika 26/Oct/2017. Vilevile aliwaomba wananchi wa Lamu wajitokeze kupiga kura kwa wingi na kwa amani ifikapo siku hiyo. Pia alisistiza watu wampigie kura Mheshimiwa Uhuru Kenyatta ili aweze kutekeleza na kumalizia miradi iliyokuwa imeanzishwa.

Trackback from your site.

Leave a comment

*