Udhamini wa LAPPSET kwa Wanafunzi wa Lamu

Serikali ya kaunti ya Lamu yashirikiana pamoja  na shirika la Lapsset kuwamotisha vijana wa Lamu waliofaidika na udhamini wa kimasomo kupitia ukanda wa Lapsset.


Katika mkutano uliofanyika tarehe 19/12/2017  ndani ya ukumbi wa lamu fort, wanafunzi waliofuzu pamoja na wale wanaondelea na masomo yao kupitia ufadhili huo, walijumuika na maafisa wa serikali kuu, viongozi wa kaunti ya Lamu Naibu gavana bwana Abdulhakim Bwana, Waziri wa Ardhi Bi Fahima Arafat, baadhi ya maafisa wa kaunti ya Lamu na maafisa wa shirika hilo.

Wanafunzi hao waliahidiwa kuwepo kwa nafasi za kujipatia mafunzo ya kikazi wanapokuwa katika masomo yao na vilevile nafasi za kazi katika mradi wa bandari ya Lamu unaotarajiwa kuwa tayari mwanzoni mwa mwaka 2018.
Naibu wa gavana Bw. Abdulhakim Bwana , aliwasihi vijana hao kujiepusha na janga hatari la mihadarati linalokera vijana wa Lamu na kuwataka waweze kuwa na mipangilio bora ya kimaisha.

Katika hadhara hiyo Bi. Fahima alipendekeza  viongozi wa Wadi katika Bunge la Lamu kupitisha mswada wa 70% ya wafanyikazi watakao ajiriwa katika bandari hiyo iwe ni wakaazi wa Lamu.

Trackback from your site.

Leave a comment

*