Usafishaji wa ufuo wa bahari 12/12/2017

Waziri wa uvuvi,mifugo na maendeleo ya ushirika kaunti ya Lamu Abdu Godana ameongoza shughuli ya kusafisha ufuo wa bahari ya kaunti hii alasiri ya leo. Godana akiwa na mafisa wengine kutoka idara hiyo pamoja na naibu wa kamishna wa kaunti ya Lamu Philip Oloo na baadhi ya wakaazi wa Lamu wengi wao wakiwa wavuvi waliojitolea waliweza kuokota taka nyingi katika ufuo huo wa bahari zikiwemo plastiki na mifuko. Akiongea na wanahabari Godana ametoa wito kwa wakaazi wa Lamu kutotupa taka kiholela baharini. Shughuli hii imefanyika mbele ya mashindano ya uvuvi hapo kesho.

Trackback from your site.

Leave a comment

*