Author Archive

WAFUGAJI WA MOA WAPA JOSHO LA NGOMBE

Wafugaji Wa Moa Wapata Josho La Ng’ombe

Wafugaji wa Moa wapokea kwa furaha cattle dip iliyofunguliwa rasmi na gavana Issa Timamy hapo jana 04/07/2017.

Kulingana na daktari wa mifugo eneo la Lamu magharibi George Kiaga amesema zaidi  ya ng’ombe 6000 wanatarajiwa kufaidi na dip hiyo.

Mradi huu utasaidia mifugo kuwakinga na mbuno na kupe ambao wanatatiza sana mifugo katika sehemu hiyo.

Pia daktari Kiaga amesema kando na kuwaogesha ngombe hao, huwa wanawapatia chanjo za kuwakinga na ugonjwa wa nimonia kwa mifugo, ugonjwa ambao zaidi unawaathiri mifugo katika eneo hilo ambalo mara nyingi hupokea mifugo kutoka kaunti jirani za Garissa na Tana riva.

Wakati wa hafla hiyo gavana Issa Timamy alipeana dawa za mifugo kwa wafugaji na kuwahimiza wafugaji hao kuitumia vyema cattle dip hiyo.

Gavana aliiyomba jamii ya wafugaji kuishi kwa amani na utangamano.

Ujenzi Wa Sehemu Ya Kujifungua Kina Mama Hospitali Ya Mpeketoni

Gavana wa kaunti ya Lamu Issa Timamy mnamo tarehe 01/07/2017 ameweka jiwe la msingi ili kujenga sehemu ya kujifungua kinamama katika hospitali ndogo ya kaunti huko Mpeketoni.

Sehemu hiyo ya kujifungulia kina mama ya ghorofa, itakuwa na uwezo wa kupokea wazazi zaidi ya 30 na kugharimu takriban shilingi milioni 50 za Kenya.

Jengo hilo la kisasa pia litakuwa na chumba chake cha upasuwaji na pia sehemu ya kina mama kujifungua kwa njia ya kawaida.

Aidha gavana Timamy alikabidhi sehemu ya ardhi katika hospitali hiyo ya Mpeketoni kwa mwanakandarasi ili  kujingwa sehemu ya kufulia nguo za hospitali kabla ya kupanda mti kwenye ardhi ya hospitali hiyo.

Pia alitembelea shule ya upili ya wavulana ya Mpeketoni kukagua ujenzi unaoendelea wa maktaba ya kisasa shuleni humo.

Upimaji Wa Mji Wa Witu

Gavana wa Lamu Issa Timamy hapo jana 03072017 alizindua rasmi upimaji na upangaji wa mji wa Witu katika eneo la Kamkunji.

Shughuli hii inatarajiwa kukamilika kwa mda wa mwezi mmoja huku wakaazi 2500 wakitazamiwa kunufaika na upimaji huu.

Zoezi hili litajumuisha nyumba za zamani za mji wa Witu na zile za mji mpya.

Gavana Timamy ameitaka kamati iliyochaguliwa kusimamia zoezi hilo kuhakikisha kuwa usawa na haki umetendeka bila ya ubaguzi.

Aidha amewaonya wale walionyakua ardhi kuwa ardhi hizo zitagawiwa wenyeji na kusema kuwa si haki kwa mtu mmoja kuchukua sehemu kubwa ya ardhi huku wengine wakiwa hawana hata kipande.

Wakati huo huo gavana Timamy alitembelea eneo la Kitumbini na kuahidi kukarabati eneo la kuogeshea ngombe ambalo limeachwa kwa miaka mingi.

Zahanati ya Muhamarani Wadi ya Mkunumbi

Zahanati hii ya Muhamarani ina hudumia watu wa sehemu ya Poromoko,Salama,Juhudi, Marafa,Mikinduni,Nyatha na Kaisari.

Kabla ya kujengwa kwa sehemu hii ya kujifungulia akinamama , kina mama wa sehemu hizi walikuwa wakitembea umbali wa kilomita 10 hadi 15 wanapotaka kujifungua na endapo kumetokea tatizo jambo ambalo lilikuwa linahatarisha usalama wa kina mama.

Gavana wa Lamu Issa Timamy aliwahimiza kina mama wajifunguwe hospitali ili wawezi kupata usaidizi wakati shida inapotokea.

Kadhalika gavana Timamy aliahidi kutoa shilingi elfu kumi kwa mama wa kwanza mja mzito atakaejifungua katika zahanati hiyo.

Zahanati ya Sinambio katika wadi ya Hongwe-Mpeketoni

Kufunguliwa kwa zahanati ya Sinabio katika wadi ya Hongwe tarafa ya Mpeketoni kumefikisha zahanati nane ambazo zimejengwa chini ya uongozi wa msatahiki gavana wa kaunti ya Lamu Issa Timamy.

Jengo la zahanati hiyo lilianza kujengwa na shirika moja la Rotary Club kutoka Italia na kushindwa kulikamilisha kwa sababu za kiusalama mnamo mwaka wa 2013.

Ukarabati wa jengo hili la zahanati uligharimu serekali ya kaunti ya Lamu shilingi milioni 8 katika mwaka wa kifedha wa 2016/2017.

Baada ya kukaa kwa mda kwa jengo hilo likiwa halikukamilika, serekali ya kaunti ilingilia kati na kulikarabati pamoja na kuweka vifaa ili iweze kupeana huduma kwa wakaazi wa Sinabio na maeneo mengine karibu.

Mara tu baada ya kufunguliwa rasmi  kwa zahanati hiyo na msatahiki gavana Issa Timamy huduma zikaanza kutolewa kwa wakaazi wa eneo hilo.

Zahanati hiyo ina chumba cha kujifungulia akina mama na iko na wahudumu wa afya wawili.

Mabingwa wa kombe la gavana 2017

Timu ya wadi ya Mkomani ndio mabingwa wa mchuwano wa Kombe la gavana kaunti ya Lamu mwaka huu baada ya kuinyuka wadi ya Bahari ambao walikuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo,mabao matatu kwa mawili.

Mnamo dakika za mwanzo timu ya Bahari ilianza kuona lango na kufunga bao kupitia kwa Viterles kabla ya kukombolewa na Ahmed Athman wa timu ya wadi ya Mkomani.

katika kipindi cha pili Mahmud Athman alifungia timu ya Mkomani wadi bao la pili kabla ya kusawazishwa na Irungu wa timu ya Bahari.

Naye Issa Islam wa timu ya wadi ya Mkomani aliifungia timu yake bao la ushindi.

Ni mwaka wa tatu sasa tangu Kombe la gavana kaunti ya Lamu kuanzishwa na mstahiki gavana Issa Timamy.

Mwaka huu timu 160 ziliweza kushiriki dimba hili kutoka wadi 10 zaka kaunti ya Lamu.

mshindi alijiondokea na shilingi laki moja pesa taslim,mpira na jezi.

“Mungu akipenda mwakani fainali za Kombe hili la gavana zitachezwa huko Faza, Lamu Mashariki” Gavana Issa Timamy aliahidi.

Kauli mbiu ya Kombe la gavana Issa Timamy kaunti ya Lamu ni kuwaleta vijana pamoja na kuwahamasisha kutojiingiza katika utumizi wa dawa za kulevya.

Idara ya afya kaunti ya Lamu yapiga hatua kubwa

Sekta ya afya ni moja wapo ya sekta ambazo zimegatuliwa kutoka serekali ya kitaifa hadi zile za kaunti.

Kwa sababu hii serekali za kaunti zimetekwa jukumu la kusimamia sekta ya afya katika kila kaunti humu nchini.

Serekali ya kaunti ya Lamu ikiongozwa na msatahiki gavana Issa Timamy imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mwananchi haswa yule aliyoko mashinani amepata huduma ya matibabu popote alipo.

Kufikia sasa serekali ya kaunti ya Lamu imejenga na kuzifungua zahanati  nane katika maeneo mbali mbali ya kaunti ya Lamu huku nyingine mbili zikielekea kukamilika.

Zahanati hizi haswa zimejengwa katika maeneo ambayo wakaazi wake walikuwa wakitembea mwendo mrefu kutafuta matibabu na ni sehemu ambazo zilitengwa kwa mda mrefu.

Zahanati za hivi karibuni zilizofunguliwa rasmi na mstahiki gavana Issa Timamy ni ile ya uziwa na tewe tarafa ya Mpeketoni.

Nyingine ni Moa,Kastakakairu,Sinabiu, Maisha Masha na Ishakani huku zile za Bargoni na Kiangwi zikielekea kukamilika.

Zahanati hizi na zile yengine zilizotangulia kufunguliwa zina uwezo wa kujifungua akina mama kwani zimetegewa chumba maalum kwa shughuli hiyo kando na kutoa huduma nyingine.

Makala Ya Mashine Za Boti Kwa Wavuvi Wa Lamu

Asilimia 80% ya wakaazi wa Lamu , hutumia uvuvi kama kitega  uchumi na raslimali  ya maisha yao.  Hivo basi kila kijiji cha kaunti ya Lamu mashariki, kimebobea kwa aina yake ya uvuvi, kama vile kiji cha kizingitini na kiwayuu  ni maarufu kwa uvuvi  wa kamba mawe na samaki wakubwa, kijiji cha Faza mbwajumwali na mtangawanda umaarufu wao ni wakuvua kaa na aina nyengine ya samaki.  Upande wa Lamu magharibi, eneo la matondoni linafahamika kama kambi ya uvuvi wa kamba wadogo.

serikali ya kaunti ya Lamu imepiga hatua katika kuboresha rasli mali hyo kupitia njia mbalimbali, ila katika makala ya leo nataka tuzungumzie mashine za boti zilizoweza kutolewa na kaunti ya Lamu kupitia idara ya uvuvi na mifugo kwa njia ya mkopo.

Takriban mashine 83 ziligawanyiwa wavuvi kupitia vyama vya BMU, vilivoko katika maeneo 19 ya  kaunti ya Lamu. Maeneo kama Shanga Rubu, Kiwayuu, Bandari salama, Siyu, Shanga Ishakani, Ndau, Myabogi, Mkokoni, Ishakani, Mbwajumwali, Kipungani, Pate, Matondoni, Kiunga, Shela, Faza, Amu na Kizingitini ndio walioweza kufaidika kwa mashine hizo.

 

Eneo la kizingitini ndilo lilopata mgao mkubwa wa mashine 16 kutokana na idadi kubwa ya wavuvi katika kijiji hicho huku maeneo ya amu na Faza ndio yaliofwata katika mgao kwa kupata  mashine 12 na maeneo yaliyobaki wakatunukiwa mashine 11.

Takriban asilimia  87% ya wavuvi waliopata mashine hizo wameweza kulezea faida kubwa wanayoipata kupitia mashine walizopewa katika shughuli zao za uvuvi, utafiti unaeleza kuwa wavuvi hao wamekuwa wakiweza kufikia maeneo yalio mbali kuvua samaki huku kiwango cha kupatikana kwa samaki kikiwa kimeongezeka kwazaidi ya kilo 20, vile vile wavuvi hao wameweza kupunguza mda wa usafiri kwa dakika sitini ikilinganishwa na zamani walipokuwa wakitumia matanga kwa usafiri wao.

Kulingana na idara husika, mradi huo utakuwa ukiendelea kila uchao kwa faida ya wavuvi wa Lamu.

The Extraction of Gas in Lamu to Start Soon

Zarara Oil and Gas Limited Company officials and Lamu governor Issa Timamy visited Faza Island on Wednesday 10th May and meet with the locals to sensitized on the progress of the planned exploration of gas.

The company is expected to drill around 1 or 2 wells in Lamu East constituency to extract gas.

Company community liaison officer Alawy Abzain said the company conducted surveys between 2012 and 2013 of block L4 in Pate island of Lamu East constituency which he said confirmed that the area had gas deposits.

The first phase of extraction will start before the end of June while the second phase is set before December.

Mr. Zain said all families that will be affected during the drilling process will be compensated.

“Discussions are already ongoing for those whose land will be used for the same. We want to ensure they are compensated,” said Mr. Zain

Mr. Zain expressed a lot of appreciation to the Lamu governor Issa Timamy and Lamu county commissioner Joseph Kanyiri for their support.

Lamu Governor Issa Timamy lauded the move for Zarara Company to commence oil and gas extraction in Lamu and assured the investors maximum cooperation.

The company has agreed to rehabilitate the road from Mtangawanda to where the oil will be extracted.

Bahati Njema

Mstahiki Gavana Issa Timamy akiandamana na naibu wake Eric Mugo, wazir wa elimu, biashara utamaduni na michezo Bw. Khamis Kaviha pamoja na afisa mkuu wa elimu Bi. Hafswa Diffini wakifungua rasmi Shule ya Chekechea katika kijiji cha Bahati njema eneo bunge la Lamu magharibi.

Shule hiyo ni ya kipekee kati ya shule zote za ECD zilizojengwa chini ya utawala wa mstahiki gavana Issa Timamy kwa kuwa ni shule iliyokamilika.

Kwa mda mrefu jamii ya Wasanye wamekuwa hawana shule yenye majengo ya kudumu ambao walikuwa wakisomea katika shule iliyojengwa kwa udogo na kuezekwa kwa makuti.

Sasa wakaazi wa sehemu hiyo wametoa wito kwa serekali kuhakikisha kuwa ardhi iliyopo shule hiyo isajiliwe rasmi na serekali.

Aidha gavana Timamy amewahakikishia wakaazi wa sehemu hiyo kuwa hawatafurushwa na mtu yoyote.

Ardhi hiyo inadaiwa kuwa imenyakuliwa na watu binafsi na tayari washatoa hati miliki.

Ni wakati huo huo gavana timamy alitawazwa kama mzee wa kisanye.