Suluhu ya maji eneo bunge la lamu masharikiSuluhu ya maji eneo bunge la lamu mashariki

“kila nyumba iungwe maji safi ya kunywa” hiyo ni kauli yake Gavana wa Lamu Mh. Fahim Twaha. Eneo bunge la Lamu Mashariki ni moja wapo ya maeneo yanayo shuhudia tatizo la maji tamu ya mfereji.

Lakini sasa tatizo hilo litazikwa katika kaburi la sahau. Hii ni baada ya jopo zima linalo shughulikia maswala ya maji Lamu LAWASCCO likiongozwa na Mkurugenzi Bw. Paul Wainaina kuzuru eneo bunge hilo kutafuta suluhu ya kudumu.


Comments are closed.

Translate »