ONYO KUHUSU MAWIMBI NA UPEPO MKALI BAHARINI

Mamlaka ya Bahari Kenya yaani Kenya Maritime Authority imetoa tahadhari ya upepo mkali na mawimbi katika Bahari Hindi.

Idara hii inaonya kuwa, hii Leo Ijumaa tarehe 3/6/2022 na hapo kesho Jumamosi 4/6/2022 Upepo utakuwa mkali sana huku kasi yake ikipungua kiasi tarehe 5/6/2022 na tarehe 6/6/2022 .

Upepo huu utakuwa tishio kwa wavuvi ambao wataendesha shughuli katika bahari, kwani unaweza kuzamisha mashua na boti ndogo.

Serikali ya Kaunti ya Lamu inawashauri wakaazi wote Lamu, wavuvi, wasafiri na hata watalii kuwa macho na kufuatilia ushauri kutoka kwa Idara ya Utabiri wa Hali ya anga pamoja na Mamlaka ya Bahari .

Serikali ya Kaunti ya Lamu kupitia Kitengo Cha Fisheries/ Blue Economy inafuatilia kwa karibu swala hili na tutaendelea kukujulisha mengi zaidi.