Waziri Mpya wa Afya Bw. Raphael Munywa Achukua Usukani

Waziri mpya wa Afya,mazingira na usafi wa jamii Bw. Raphael Munywa hapo jana alikabidhiwa rasmi mamlaka na mtangulizi wake anayeondoka Dakatari Mohamed Kombo katika majengo ya hospitali ya King Fahad kaunti ya Lamu.

Akizungumza wakati wakumkabidhi rasmi mamlaka waziri huyo mpya, daktari Kombo alieleza matumaini yake na imani yake kwa serekali ya sasa kwa kuboreshwa kwa hospitali za Lamu zaidi, na kueleza kuwa yeye binafsi aliwahi kufanya kazi na gavana wa sasa Fahim Yassin Twaha alipokuwa mbunge wa Lamu magharibi na kumtaja kuwa alikuwa mchapa kazi.

Na kwa upande wake waziri Munywa amempongeza daktari Kombo kwa bidii yake na kusema kuwa bado atashirikiana naye ili kusaidia watu wa Lamu na kuahidi kuwa ataboresha huduma katika hospitali hiyo.
Hafla hiyo imehudhuriwa na wafanyikazi na wakuu wa idara mbali mbali za afya pamoja na wakaazi wa Lamu.