Mstahiki Gavana Issa Timamy mapema hii leo, ametoa takriban shilingi laki 5 kufadhili Kombe la Mfungo na Kilabu ya King loyal ya Kizingitini, iliojikatia nafasi ya kushiriki ligi ya Mikoa baada ya kufuzu Katika michuwano iliyoandaliwa na Shirikisho la Kandanda Nchini tawi la Lamu.
Michuwano hii ya Kombe la Mfungo inaandaliwa kwa timu za Kipungani, Matondoni, Mokowe,Uwanja wa Mala kwa Vijana chini ya miaka 13 na 17,Soka ya ufukweni Wiyoni-Lamu, Uwanja wa Sposi kwa wenye umri wa Zaidi ya miaka 35,Timu za watu 7 kila upande kwa wachezaji waliozidi miaka 40 pamoja na Uwanja wa Twaifu.
Akiwakabidhi hundi hizo afisini mwake, Gavana Timamy, ameahidi kuendelea zaidi kuwasaidia vijana katika michezo kwa nyanja zote kama alivyowasaidia waogeleaji.
Aidha, Gavana Timamy, amesema nia yake ni kuona kuwa viwanja vyote katika Kaunti ya Lamu vimeboreka.
Waliokuwepo ni pamoja na Afisa mkuu wa wafanyikazi Abdinassir Issa, Waziri wa Elimu Sebastian Owanga pamoja na afisa mkuu wake Hafswa Difini.