Takriban marefarii 30 waliochini ya umri wa miaka 35 Kutoka Kaunti ya Lamu, wanapokea mafunzo ya class 3 ya kuchezesha mpira wa miguu ili waweze kujiunga na wenzao waliohitimu kuchezesha ligi za majuu.

Mafunzo hayo ya wiki moja, yamedhaminiwa na serekali ya Kaunti ya Lamu, ambapo imeleta Refarii mkufunzi aliyehitimu na kuidhinishwa na Shirikisho la Soka duniani.

Akifungua Rasmi warsha hiyo, Waziri wa Michezo Sebastian Owanga, amesema wamefikia hatua hiyo, kufuatia ripoti ya diba lililochezwa la Talanta Hela, ambapo iliyoonyesha kwamba kuna dosari katika marefarii na wakufunzi wasoka Lamu.

Aidha Owanga, amesema mafunzo hayo yatasaidia kuenua kiwango cha mpira wa kabumbu Kaunti ya Lamu na hata kupunguza utumizi wa dawa za kulevya kwa vijana.

Waliokuwepo ni pamoja na Afisa mkuu wa Michezo Hafswa Difini, Mkurugenzi wa Michezo Peter Ndichu pamoja na Afisa wake Abubakar Basalama.