Idara ya Elimu Vijana,Jinsia Huduma za jamii na Michezo, imeandaa mkutano wa wadau wa sekta ya Michezo kutoka kila wodi ili kutathmini hali ya Michezo pamoja na changamoto zilizopo.

Ukosefu wa viwanja bora pamoja na malumbano ya uongozi zimetajwa kama kati ya changamoto zinazoregesha nyuma sekta mzima ya Michezo.

Akizungumza Na wadau katika mkutano huo, Waziri wa Elimu, Vijana, Jinsia, Huduma za jamii na Michezo Sebastian Owanga, amemuamuru Mkurugenzi wa Michezo Bw. Peter Ndichu, kuunda sajili ya klabu zote za Michezo zilizopo katika Kaunti ya Lamu pamoja na wanachama wake kabla ya tarehe I Juli mwaka huu .

Aidha, Bw. Owanga amesema, ili Michezo kuimarika katika Kaunti hii, lazima Sheria ya Kaunti ya Michezo ya mwaka 2018 itumike ipasavyo.

“Tafadhali tusaidiyani kuweka nidhamu kwenye Michezo, Na sheria hii itasaidia pakubwa katika kulainisha mambo kadhaa” Waziri huo aliongezea.

Waliokuwepo ni pamoja na Afisa mkuu wa Michezo Bi. Hafswa Difini pamoja na Afisa wa Michezo Abubakar Basalama.