Waziri wa Madini, Uchumi Samawati na Shughuli za Baharini Muhishimiwa Salim Mvuriya amewasili katika kaunti ya Lamu kwa ziara rasmi ya kiserekali.
Waziri Mvuriya amepokelewa na mwenyeji wake Muhishimiwa Issa Timamy ambaye pia ni mwenyekiti wa Uchumi Samawati katika baraza la magavana nchini akiwa ameongozana na wakuu mbali mbali serekalini.
Ziara yake Mvuriya itajumuisha:-
– Mpango wa kuanzisha kituo cha mafunzo ya mambo ya Baharini
– Uwasilishaji wa kuonyesha nafasi za uwekezaji zilizopo Katika kaunti ya Lamu.
– Mapendekezo ya miradi tofauti inaofaa kufanyika.
– Shughuli ya Upanzi wa miti eneo la Maisha masha ikiwa ni kutekeleza agizo la rais William Samoei Ruto.
– Mwisho –