“Mazingira na Maslahi ya Kijamii kupewa kipao mbele kwenye Mradi unaofadhiliwa na Banki ya Dunia”.
Mradi wa kuboresha makaazi yasiorasmi nchini Kenya unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, utahakikisha kuwa mazingira na maslahi ya ulinzi wa Kijamii yameshughulikiwa ipasavyo ili kuzuwia maafa na migogoro.
Timu ya Kitaifa ya Uratibu wa Mradi(NPCT)na ile ya Kaunti (CPCT)pamoja na Mshauri kutoka kwa Benki ya Dunia, wametembelea makaazi yasiorasmi yaliyoratibiwa kuboreshwa katika Kaunti ya Lamu kwa zoezi la uthibitishaji wa mazingira na maslahi ya ulinzi wa Kijamii yametiliwa maanani ili mradi uwende sambamba na kanuni zilizowekwa kutekeleza Mradi huo unaodhaminiwa na benki ya Dunia kwa ushirikiano na serekali ya Kitaifa na ile ya Kaunti.
Shughuli za kibiashara, makaazi pamoja na usalama zinatarajiwa kuimarika mara tu mradi huu utakapokamilika.
Mradi huu, unalenga kuboresha makaazi yasiorasmi nchini kwenye Kaunti 33 huku Kaunti ya Lamu ikiwemo, ambapo makaazi yasiorasmi kama vile Witu, Mokowe,Matondoni, Wiyoni,Faza na Kiunga yatanufaika na Mradi huo.