Idara ya Afya kaunti ya Lamu itashirikiana na washikadau mbalimbali ili kufanikisha Mpango wa Utunzi wa Afya ya msingi almaarufu kama Primary Health Care ulioanzishwa na Serekali ya Kitaifa chini ya Kauli mbiyu Afya yetu jukumu letu.

Kulingana na Naibu Mkurugenzi wa Afya humu nchini ambaye pia ni msimamizi Wa Kitengo cha Utunzi wa Afya Msingi, Daktari Salim Ali Hussein, amesema kwamba mpango huu unalenga kuwezesha kufikia lengo la kupeana huduma kwa wote.

Pia mpango huu, utawezesha kukinga Na kupunguza magonjwa na vifo vinavyotokana na magonjwa ya kuambukiza.

Aidha Daktari Hussein, ametioa wito kwa washikadau kushirikiana ili kufanikisha mpango huu wa kupeleka afya mashinani.

Gavana wa Lamu Issa Timamy, mapema mwaka huu alizindua huduma ya kutibu watu mashinani ambao inafahamika Kama “Timamy Care” Chini ya Kauli mbiyu Afya mashinani,Afya majumbani.