Wizara ya Elimu hii leo, imeandaa warsha ya kuhamasisha vijana ili kujiunga na Chuo cha Kiufundi cha Kizingitini kwa taaluma mbalimbali.
Warsha hii, imefanyika Katika Ukumbi wa Kijamii Wa Pate iliyowaleta pamoja vijana wa Mtangawanda, Pate,Siu,Shangarubu na Shangaishakani,huku warsha iliofanyika Katika Ukumbi wa Kijamii Wa Rasini ikijumuisha vijana wa Tchundwa,Mbwajumwali,Myabogi,Kizingitini na Rasini.
Akizungumza na vijana hao ambao wengi wamekamilisha masomo ya sekondari , Waziri wa Elimu Sebastian Owanga,amewataka vijana kutumia fursa ya kujipatia ujuzi wa kazi za mkono kwenye Chuo hicho cha Kizingitini, kwa kuwa serekali ya mstahiki Gavana Issa Timamy inagharamikia masomo hayo kwa ujumla.
Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na ufundi umeme,seremala,ususi na urembo ,ufundi cherehani na ufundi mfereji.
Vijana kadhaa walitumia fursa hiyo na kujisajili baada ya kukamilika kwa warsha hizo huku usajili ukiendelea.
Waliohudhuria warsha hiyo ni pamoja na Afisa mkuu wa Elimu Bi.Afswa Difini, Afisa mratibu wa vijana Mohamed Kassim,Afisa Wa michezo Peter Ndichu miongoni mwa maafisa wengine.