Mstahiki Gavana Issa Timamy akutana na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Usambazaji wa Umeme vijijini na nishati mbadala, Bw. Godfrey Lemiso na kujadili njia za ushirikiano ili kuimarisha na kupeana huduma bora kwa wananchi.

Miongoni mwa waliojadili ni pamoja na:-

– Kukwamua changamoto kutoka kwa mradi wa kusambaza umeme huko Manda.

Kuweka umeme wa kutumia paneli za jua katika maeneo ya Mkokoni, Kiwayuu na Ndau.

– Ushirikiano wa gharama ya pamoja kati ya serekali ya kaunti ya Lamu na Shirika la Usambazaji wa Umeme vijijini na Nishati mbadala.